1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya watu 40 wauawa katika mashambulizi DRC

15 Aprili 2023

Zaidi ya watu 40 wameuawa katika mashambulizi yaliyovilenga vijiji kadhaa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, yanayodaiwa kufanywa na kundi la wanamgambo wa CODECO.

https://p.dw.com/p/4Q85K
Demokratische Republik Kongo, Mindestens zehn Tote bei Anschlag auf Kirche in Kasindi
Picha: Zanem Nety Zaidi/Xinhua/IMAGO

Kundi hilo linatuhumiwa kuvishambulia vijiji vitatu katika jimbo la Ituri, umbali wa kilomita 60 kutoka mji mkuu wa jimbo wa Bunia.

Wanamgambo wa CODECO wanadai kwamba wanailinda jamii ya Lendu kutoka kabila jingine la Hema na jeshi.

Msimamizi wa mkoa Innocent Matukadala, amelieleza shirika la habari la AFP kwamba wameipata miili ya watu 36 katika eneo la Kilo Etat na mingine 8 ilipatikana katika eneo la Matete.

Kiongozi mwingine wa mashirika ya kiraia katika wilaya hiyo hiyo Robert Basiloko amesema idadi ya waliouawa ni 43, watoto wakiwa miongoni mwa wahanga.