1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya Wapalestina 20,000 waelezwa kuuwawa Gaza

22 Desemba 2023

Wizara ya afya inayoendeshwa na kundi la Hamas imesema idadi ya watu waliokufa katika Ukanda wa Gaza imeongezeka na kufikia 20,057.

https://p.dw.com/p/4aTQx
Gazastreifen | Israelische Offensive
Picha: Abed Rahim Khatib/dpa/picture alliance

Idadi hiyo inawakilisha karibu asilimia moja ya wakaazi wa eneo hilo kabla ya mapigano hayo kuanza.Wizara hiyo ya afya imeongeza kuwa zaidi ya watu 53,000 wamejeruhiwa huku asilimia 85 ya watu milioni 2.2 wa Gaza wamelazimika kuyahama makaazi yao. Wizara hiyo ya afya haitofautishi kati ya raia na wapiganaji waliojeruhiwa japoimeeleza kuwa, idadi kubwa ya waliopoteza maisha ni wanawake na watoto. Israel yenyewe wakati mwengine imetilia shaka juu ya uaminifu wa takwimu za vifo na majeruhi zinazotolewa na wizara hiyo ya afya inayoendeshwa na Hamas.