1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IPC yaonya kitisho cha baa la njaa Gaza

22 Desemba 2023

Ripoti ya taasisi ya kimataifa inayokadiria viwango vya upatikanaji wa chakula - IPC inaonya kuhusu kuzuka kwa baa la njaa katika Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4aSwh
Gazastreifen I Palästinenser tragen Lebensmittel in der Nähe eines vom Palästinensischen Flüchtlingswerk der Vereinten Nationen (UNRWA) betriebenen Lagers in Khan Younis
Picha: Ibraheem Abu Mustafa/REUTERS

Kulingana na ripoti hiyo, wakaazi milioni 2.3 wa Ukanda huo kwa sasa wanakabiliwa na viwango vya juu vya uhaba mkubwa wa chakula. Ripoti hiyo pia imesema hali hiyo huenda ikawa mbaya zaidi kama mambo yataendelea kusalia kama yalivyo kwa sasa. Shirika hilo la IPC linaloungwa mkono na Umoja wa Mataifa limesema mazingira ya njaa bado hayajashika kasi. Limetajakipindi kifupi ambapo watu wamekabiliwa na utapiamlo. Hata hivyo, IPC imeonya kuna uwezekano mkubwa mabadiliko haya yanaweza kutokea kama hali haitaimarika. Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Ujerumani imeyataja makadirio hayo ya IPC kuwa ya kutisha.