1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaFinland

Zaidi ya waomba hifadhi 200 waingia Finland wakitokea Urusi

15 Desemba 2023

Walinzi wa mpakani wa Finland wamesema leo zaidi ya watu 200 wanaotafuta hifadhi wameingia nchini humo wakitokea Urusi tangu nchi hiyo ilipofungua tena baadhi ya mipaka yake kwa muda baada ya kufungwa kwa wiki mbili.

https://p.dw.com/p/4aDy5
Eneo la mpaka baina ya Finland na Urusi
Eneo la mpaka baina ya Finland na Urusi Picha: Otto Ponto/Lehtikuva/AFP

Serikali ya Finland ilieleza jana kuwa, itaufunga mpaka wake kuanzia saa kumi na mbili leo jioni, wakati huu wakiufunga mpaka wake na Urusi kwa muda wa mwezi mmoja kufuatia ongezeko la watu wanaotafuta hifadhi nchini humo.

Waomba hifadhi wapatao 900 kutoka Kenya, Morocco, Pakistan, Somalia, Syria na Yemen wameingia Finland wakitokea Urusi mwezi uliopita.

Mamlaka mjini Helsinki inasema ongezeko hilo la waomba hifadhi wanaotokea Urusi ni mbinu mojawapo ya Urusi ya kulipiza kisasi kutokana na uamuzi wa Finland wa kuimarisha ushirikiano wa ulinzi na Marekani. Hata hivyo ikulu ya Kremlin imekanusha madai hayo.