1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yakanusha kupeleka wakimbizi Finland

20 Novemba 2023

Urusi imekanusha madai kwamba inapeleka wahamiaji katika mpaka wa Finland, baada ya taifa hilo kuripoti idadi kubwa ya waomba hifadhi wanaojaribu kuingia nchini humo kinyume cha sheria.

https://p.dw.com/p/4ZEf2
Kremlin | Msemaji wa Ikulu ya Urusi Dmitry Peskov
Msemaji wa Ikulu ya Urusi Dmitry PeskovPicha: Mikhail Tereshchenko/TASS/dpa/picture alliance

Finland ilifunga mipaka yake minne na Urusi wiki iliyopita kufuatia kuongezeka kwa idadi ya waomba hifadhi, na kuituhumu Moscow kwamba inajaribu kuiyumbisha nchi hiyo kufuatia hatua yake ya kujiunga na Jumuiya ya kujihami NATO. 

Msemaji wa Ikulu ya Urusi Dmitry Peskov aliwaambia waandishi habari kuwa Urusi haitokubali madai kama hayo, akisema vivuko vya mpakani  vinatumiwa na wale walio na haki ya kufanya hivyo. 

Soma pia:Urusi imefanya mashambulizi dhidi ya Ukraine baada ya wiki kadhaa ya kusimamisha mapigano

Alexander Grushko Naibu waziri wa mambo ya nje wa Urusi amesema uamuzi wa Finland kufunga mipaka yake unakinzana na masilahi ya taifa hilo.

Mahusiano ya mataifa hayo mawili yameingia doa tangu Urusi ilioanzisha uvamizi wake nchini Ukraine mwaka uliyopita.