1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ZAGHREB: Mahakama ya jinai huko The Hague na shughuli zake.

16 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFWV

Umoja wa Ulaya huenda ukachelewesha kuanza kwa mazungumzo na Croatia hadi utawala wa Zaghreb utakapo mtoa mshukiwa mkuu wa uhalifu wa vita, Generali Ante Gotovina mtuhumiwa mkuu wa uhalifu wa kivita ili afikisbhwe mbele ya mahakama ya umoja wa mataifa huko The Hague kwa tuhuma za kuwauwa wasarbia takriban 150 wakati wa vita vya Croatia kati ya mwaka 1991 na 1995.

Wakati huo huo mahakama hiyo ya jinai ya kimataifa huko The Hague imeanza rasmi kikao cha kwanza katikacho tuama juu ya uchunguzi kuhusu uhalifu uliotekelezwa katika mapigano ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kikao hicho ni cha kwanza kuwahi kufanywa na mahakama hiyo katika kipindi cha miaka kumi tangu kufunguliwa kwake.

Hatua inafuatia kuyumbayumba kwa hali ya usalama nchini Kongo kutokana na vita vya miaka mingi vya wenyewe kwa wenyewe.

Kiongozi wa mashataka wa mahakama ya The Hague Luis Moreno Ocampo mwaka uliopita alianzisha uchunguzi wake juu ya alichokitaja kuwa uhalifu wa hali ya juu uliohusisha mauaji ya halaiki, ubakaji, na mateso mengine dhidi ya raia nchini Kongo hasa katika eneo la Ituri kaskazini Mashariki mwa Kongo.