1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Xi ataka Urusi na Ukraine kuwa na mazungumzo ya amani

8 Julai 2024

Waziri Mkuu wa Hungary Victor Orban amefanya ziara ya kushtukiza mjini Beijing katika juhudi zake za kutafuta suluhu ya amani kwa mzozo wa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4i0gG
China | Viktor Orban und Xi Jinping
Picha: China Daily via REUTERS

Rais wa China Xi Jinping amemwambia Orban kwamba mataifa yenye nguvu duniani yanapaswa kuandaa mazingira na kuzisaidia Urusi na Ukraine kuanzisha upya mazungumzo ya moja kwa moja ya amani.

Xi ameongeza kuwa matumaini ya usitishwaji vita yatapatikana pale tu mataifa makubwa yatakapokuwa na nia njema badala ya mitazamo hasi. 

Je, mkutano wa kilele wa Ukraine umefikia malengo yake?

Orban ambaye nJe, mkutano wa kilele wa Ukraine umefikia malengo yake?chi yake ndio inashikilia kwa sasa urais wa kupokezana wa Umoja wa Ulaya, alifanya pia ziara mjini Kyiv na Moscow na sasa yuko njiani kuelekea Washington ambako atashiriki mkutano wa NATO utakaoanza hapo kesho.