1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wickremesinghe achaguliwa rais wa Sri Lanka

20 Julai 2022

Wabunge wa Sri Lanka Jumatano walimchagua waziri mkuu Ranil Wickremesinghe kuwa rais wa nchi hiyo na kuchukua nafasi ya kiongozi aliyeondolewa madarakani Gotabaya Rajapaksa.

https://p.dw.com/p/4EOWq
Krisenland Sri Lanka hat einen neuen Präsidenten
Picha: Eranga Jayawardena/AP/dpa

Kura hiyo inatishia kuchochea msukosuko wa kisiasa katika taifa hilo la kisiwa. Baada ya kura hizo zilizokuwa na ushindani, Wickremesinghe alipata kura 134 huku mpinzani wake mkuu Dulla Alahapperuma akijizolea kura 82.

Mgombea wa tatu, Anura Kumara Dissanayake, alipata kura tatu pekee kutoka kwa chama chake.

Rais wa zamani Gotabaya Rajapaksa alimteua Wickremesinghe kama waziri mkuu mwezi Mei, akitumai uteuzi huo ungeleta utulivu katika nchi hiyo ambayo inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kiuchumi.

Wickremesinghe alihudumu kama rais wa mpito baada ya Rajapaksa kuikimbia nchi wiki iliyopita na kujiuzulu kwa njia ya barua pepe.