1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiSyria

WFP kupunguza msaada wa chakula nchini Syria

14 Juni 2023

Shirika la chakula la Umoja wa Mataifa WFP limeonesha nia ya kupunguza misaada kwa Wasyria wanaohitaji chakula cha msingi kwa karibu nusu kutokana na ukosefu wa fedha.

https://p.dw.com/p/4SY3Q
Nobelpreisträger 2020 | Friedensnobelpreis | UN World Food Programme
Picha: Erik De Castro/Reuters

Shirika hilo limesema mgogoro wa kifedha ambao haujawahi kushuhudiwa unalazimisha kupunguzwa msaada kwa watu milioni 2.5 kati ya watu milioni 5.5 wanaotegemea shirika hilo kwa mahitaji yao ya kimsingi ya chakula.

WFP imesema ikiwa itaendelea kutoa msaada kwa watu milioni 5.5, itakosa chakula kabisa cha kuwapa watu ifikapo Oktoba.

Soma pia: Antonio Guterres aunga mkono kupelekwa misaada nchini Syria

Taaarifa hiyo inatolewa wakati Umoja wa Ulaya leo hii ukijiandaa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa saba wa huko mjini Brussels wenye kujikikata katika kusaidia hatma ya Syria na Kanda nzima.