1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Ujerumani ametowa mwito kutafutwa njia amani Niger

14 Agosti 2023

Waziri wa maendeleo wa Ujerumani Svenja Schulze ametowa mwito wa kuwepo njia ya amani ya kutafuta suluhisho katika mgogoro wa Niger.

https://p.dw.com/p/4V8W5
Lateinamerika und Karibik | Entwicklungsministerin Svenja Schulze
Picha: Janine Schmitz/photothek/IMAGO

Waziri huyo wa Ujerumani ametowa mwito huo kabla ya ziara yake Magharibi mwa Afrika.Amesema kuna njia nyingi tofauti za kulishughulikia suala la mgogoro huo ikiwemo kuhakikisha kunafanyika uchaguzi mpya hivi karibuni au kuachiliwa huru rais Mohamed Bazoum aliyechaguliwa kidemokrasia na bila ya kupata madhara. Schulze anatarajiwa kuwasili Mauritania ambako ni kituo cha kwanza cha ziara yake ya siku nne Afrika Magharibi na Jumatano atakwenda Nigeria ambako atafanya mazungumzo na wawakilishi wa Jumuiya ya kiuchumi ya Ukanda huo,ECOWAS. Miongoni mwa yatakayojadiliwa ni kutafuta namna ambavyo Ujerumani inaweza kuunga mkono juhudi za kutafuta suluhisho Niger.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW