1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yairai China kuachana na matumizi ya makaa ya mawe

24 Juni 2024

Waziri wa Uchumi wa Ujerumani, aliye ziarani nchini China, Robert Habeck amesema ni muhimu kwa China kufikia malengo ya uhifadhi wa mazingira duniani.

https://p.dw.com/p/4hPLW
China Hangzhou | Waziri wa Uchumi Robert Habeck nchini China
Waziri wa Uchumi Robert Habeck akiwa mjini Hangzhou nchini ChinaPicha: picture alliance/dpa

Na lazima ipate nishati salama, mbadala wa makaa ya mawe, ambayo yamechangia karibu asilimia 60 ya usambazaji wa umeme wa taifa hilo kwa mwaka 2023.

Maafisa walimwambia Habeck kwamba China imekuwa ikipanua wigo wa uzalishaji wa makaa ya mawe kwa sababu za kiusalama. Lakini Waziri Habeck alisema ushirikiano na China lazima uimarishwe na kuongeza kuwa bila taifa hilo haingewezekana haitawezekana kufikia malengo ya kimataifa.

Pamoja na upanuzi wa uzalishaji wake wa makaa ya mawe lakini pia imezalisha karibu gigawati 350 za uwezo mpya wa nishati mbadala 2023, ikiwa ni zaidi ya nusu ya jumla ya uzalishwaji wa kimataifa.