1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUjerumani

Habeck azuru China katikati ya mvutano wa ushuru wa magari

22 Juni 2024

Waziri wa Uchumi wa Ujerumani na Makamu Kansela Robert Habeck yuko Beijing kwa ziara ya siku tatu katikati ya mvutano juu ya mazungumzo ya hivi karibuni ya kuongeza ushuru wa uagizaji wa magari ya umeme ya China.

https://p.dw.com/p/4hNek
Gari linalotumia umeme
Gari ya umeme, Model S likiwa sokoni kwenye mji wa Wuhan nchini China. Taifa hilo na Ulaya wanavutana hivi sasa kuhusiana na masuala ya ushuru wa kuingiza magari kama haya barani UlayaPicha: Chen Wen/HPIC/dpa/picture alliance

Beijing:

Magari yanayoguswa kwenye mvutano huu ni ya umeme ya China yanayouzwa Umoja wa Ulaya.

Habeck ndiye waziri wa kwanza wa ngazi ya juu wa Ulaya kuzuru China tangu Ulaya ilipotangaza pendekezo hilo la ushuru.

China hata hivyo inayapinga mapendekezo hayo na kutishia vita vya kibiashara wakati watengenezaji wake wa magari wakiiomba serikali ya Beijing kusawazisha ushuru wa kuagiza magari.

China na Ujerumani wanaiona safari hiyo kama fursa kwa Habeck, kama msemaji wa taifa lenye nguvu kubwa kiuchumi Ulaya na mwenye uhusiano wa kina na soko la China.

China ilichangia karibu theluthi moja ya mauzo yote ya magari ya Ujerumani mwaka jana.