1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baerbock na washirika wa G7, wajadili yanayoendelea Urusi

24 Juni 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amezungumza na mawaziri wenzake wa kundi la mataifa saba tajiri duniani, juu ya matukio ya nchini Urusi.

https://p.dw.com/p/4T1Cj
Berlin | Aussenministerin Annalena Baerbock
Picha: Jens Krick/Flashpic/picture alliance

Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani imearifu kwamba muda mfupi uliopita waziri Baerbock, aliwasiliana na mawaziri wenzake wa kundi la  G7. Msemaji wa wizara hiyo pia ameeleza kuwa kikosi kazi cha serikali ya Ujerumani kimefanya mkutano.

Soma zaidi:Mataifa ya G7 yadhamiria kuiunga mkono Ukraine

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema uasi uliofanywa na mamluki wa kundi la Wagner unaonesha kuwa Urusi ni dhaifu. Itakumbukwa kuwa, kundi la mamluki la Wagner limekuwa likihusishwa kufanya operesheni zake katika baadhi ya mataifa ya Afrika yakiwemo Mali na Sudan.