1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baerbock ahimiza uhusiano mzuri na nchi za eneo la Pasifiki

22 Agosti 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock ametoa wito kwa Australia na nchi nyingine za eneo la bahari ya Pasific kushirikiana kwa ukaribu na washirika wa Ulaya ili kukabili sera za ushari za China

https://p.dw.com/p/4VSSm
Berlin PK Außenministerin Annalena Baerbock
Picha: Bernd Elmenthaler/IMAGO

Waziri Baerbock alisema hayo kwenye mkutano kwa njia ya mtandao na taasisi ya jopo la wataalamu la Lowy, lenye makao yake mjini Sydney nchini Australia.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani ameeleza kuwa ushirikiano huo utapaza sauti za nchi hizo na umoja wao utaongeza nguvu zao maradufu.

Marekani Japan na Australia zapanga luteka ya pamoja katika bahari ya Kusini mwa China

Amesema China imebadlika na hivyo sera za nchi hizo juu ya China pia zinapaswa pia kubadilika.