1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza ziarani Ukraine

16 Novemba 2023

Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza David Cameron ameapa kuendelea kuipa Ukraine msaada wa kijeshi.

https://p.dw.com/p/4Yrlt
Ukraine, Kyiv | Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza David Cameron mjini Kyiv
Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza David Cameron akisalimiana na rais Volodomyr Zelensky wa Ukraine mjini Kyiv.Picha: UKRAINIAN PRESIDENTIAL PRESS SERVICE/REUTERS

Cameron ameyasema hayo wakati wa ziara yake mjini Kyiv kwa mazungumzo na Rais Volodymyr Zelensky.

Waziri mkuu huyo wa zamani yuko Kyiv kwenye ziara yake ya kwanza ya kigeni kama waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza, ambayo imekuwa mshirika mkubwa wa kijeshi na kisiasa wa Ukraine tangu uvamizi wa Urusi.

Cameroon amesema Uingereza itaendeleza ushirikiano wake na Ukraine sio kwa mwaka huu tu na mwaka ujao bali kwa muda wote watakaohitaji msaada.

Zelensky amemshukuru Cameron kwa kufanya ziara hiyo katika wakati ambao ulimwengu umeugeukia mzozo unaoendelea kutokota katika Mashariki ya Kati.