1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa aahidi msaada kwa Ukraine

13 Januari 2024

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ufaransa Stephane Sejourne ameahidi kuendelea kuiunga mkono Ukraine na ushirikiano wa utengenezaji wa vifaa vya ulinzi.

https://p.dw.com/p/4bCnY
Ukraine Französischer Minister für auswärtige und europäische Angelegenheiten Stephane Sejourne zu Besuch in Kiew
Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Dmytro Kuleba azungumza na mwenzake wa Ufaransa Stephane SejournePicha: Gleb Garanich/REUTERS

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ufaransa Stephane Sejourne ameahidi kuendelea kuiunga mkono Ukraine na ushirikiano wa utengenezaji wa vifaa vya ulinzi. Sejourne ameyasema hayo leo, katika ziara yake ya kwanza ya rasmi tangu kuchukua wadhifa huo mpya wiki hii.

Soma pia: Waziri mpya wa mambo ya nje wa Ufaransa azuru Kyiv kwa mara ya kwanza

Akizungumza katika kikao cha waandishi habari mjini Kyiv, waziri huyo amesema Urusi inatumai Ukraine na washirika wake watachoka kabla ya wao lakini hilo halitatokea. Kyiv inalenga kuendelea kupokea msaada wa kijeshi na kifedha kutoka kwa washirika wake wa Magharibi baada ya karibu miaka miwili ya kupambana na uvamizi kamili wa Urusi.

Serjoune, mwenye umri wa miaka 38, aliwasili Kyiv, saa chache baada ya Urusi kufanya mashambulizi 40 ya makombora na droni nchini Ukraine. Waziri huyo wa wa mambo ya nje wa Ufaransa amesema atajitahidi katika siku na wiki chache zijazo kurekebisha masuala ya kisheria katika Umoja wa Ulaya ili kuzisaidia kampuni za Ufaransa kujenga viwanda vya uzalishaji wa vifaa vya kijeshi nchini Ukraine.