1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri mpya wa mambo ya nje wa Ufaransa azuru Kyiv

13 Januari 2024

Waziri mpya wa mambo ya nje wa Ufaransa Stephane Sejourne amewasili Kyiv Jumamosi katika ziara yake ya kwanza rasmi ya kigeni, ikiwa ni ishara ya uungaji mkono.

https://p.dw.com/p/4bCK9
Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Stephane Sejourne
Waziri Sejourne anafanya ziara yake ya kwanza ya kigeni mjini Kyiv baada ya kuchukua usukaniPicha: Thomas Padilla/REUTERS

Waziri mpya wa mambo ya nje wa Ufaransa Stephane Sejourne amewasili Kyiv leo katika ziara yake ya kwanza rasmi ya kigeni, ikiwa ni ishara ya uungaji mkono. Hayo ni wakati uvamizi wa Urusi nchini Ukraine ukikaribia mwaka wake wa pili. Wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa imesema Sejourne yuko Kyiv kuendeleza juhudi za kidiplomasia za Ufaransa na kusisitiza dhamira ya Ufaransa kwa washirika wake na kwa raia wa nchi hiyo.

Soma pia: Sunak atangaza msaada mpya wa mabilioni ya dola kwa Ukraine

Sejourne yuko Kyiv siku moja baada ya Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak kufanya ziara ya kushtukiza mjini humo na kutangaza msaada mpya wa mabilioni ya dola kwa Ukraine. Wakati huo huo, jeshi la angani la Ukraine limesema leo kuwa Urusi ilifanya mashambulizi kadhaa kote Ukriane usiku kucha. Jeshi hilo limesema jumla ya mashambulizi 40 ya adui yalirekodiwa, likiongeza kuwa liliyaharibu makombora nane.