1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiMarekani

Marekani na China zakubaliana kuweka uwanja sawa wa kiuchumi

11 Novemba 2023

Waziri wa Fedha wa Marekani Janeth Yellen amesema jana kwamba yeye pamoja na Naibu Waziri Mkuu wa China He Lifeng wamekubaliana kushirikiana ili kuwa na uhusiano bora wa kiuchumi.

https://p.dw.com/p/4YgrJ
Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen amesema baada ya mazungumzo na China wamekubaliana kuboresha zaidi mazingira ya kiuchumi na kupunguza misuguano
Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen amesema baada ya mazungumzo na China wamekubaliana kuboresha zaidi mazingira ya kiuchumi na kupunguza misuguano Picha: Mark Schiefelbein/AP Photo/picture alliance/dpa/

Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen amesema jana kwamba yeye pamoja na Naibu Waziri Mkuu wa China He Lifeng wamekubaliana kushirikiana ili kuwa na uhusiano bora  wa kiuchumi.

Yellen amesema hayo baada ya mazungumzo ya siku mbili ambayo pia yalisaidia kuweka msingi wa mkutano wa wiki ijayo kati ya Rais Joe Biden na Rais wa China Xi Jinping.

Yellen amesema pamoja na tofauti zinazosalia baina ya mataifa hayo mawili, lakini watashirikiana katika changamoto za kimataifa kuanzia madeni hadi changamoto za kiuchumi zinazoibuliwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

Amesema, mataifa hayo mawili yamekaribisha lengo la uhusiano wenye tija wa kiuchumi utakaotoa mazingira sawa ya kwa makampuni na wafanyakazi ili kuzinufaisha nchi zote mbili.