1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yellen airai China kupambana na mabadiliko ya tabianchi

8 Julai 2023

Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen aliye ziarani nchini China leo ametoa mwito kwa mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa duniani kufanya kazi pamoja kukabiliana na janga la Mabadiliko ya Tabianchi.

https://p.dw.com/p/4TcOi

Yellen alikuwa akizungumza kwenye mjadala unaondaliwa mjini Beijing kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi ambao umehudhuriwa na maafisa wa serikali ya China na wataalamu wa masuala ya mazingira.

Waziri huyo wa fedha alitumia hotuba yake kukumbusha namna ushirikiano kati ya China na Marekani ulivyosaidia kupatikana kwa mkataba wa Paris wa mwaka 2015 unatoa mwongozo na malengo ya kushughulikia mabadiliko ya tabianchi duniani.

Mbali na ushirikiano wa kisiasa, Yellen vilevile amehimiza Washington na Beijing kuunganisha nguvu kupitia michango ya kifedha ya kufadhilisha mapambano dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi duniani.