1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Abiy afanya mazungumzo na viongozi wa Sudan

27 Januari 2023

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed amefanya mazungumzo na viongozi kadhaa wa Sudan kwa nia ya kufufua uhusiano kati ya nchi hizo mbili jirani za Afrika.

https://p.dw.com/p/4MmKQ
Äthiopien | Eröffnung Freihandelszone in Dire Dawa
Picha: Mesay Tekelu/DW

Kwa miaka kadhaa, Sudan na Ethiopia zimekuwa katika mzozo kuhusu mpaka na ujenzi wa bwawa kubwa la umeme katika Mto Nile ambalo pia limesababisha mvutano na Misri ambako pia mto huo unapita. 

Soma zaidi: Bwawa kubwa la utata la Ethiopia

Ethiopia yaanza tena kujaza bwawa la Grand Renaissence

Shirika la Habari la Sudan, SUNA, limetangaza kuwa masuala kuhusu bwawa la umeme la Renaissance na mpaka yamejadiliwa katika mkutano kati ya Abiy na mkuu wa utawala wa kijeshi wa Sudan, Jenerali Abdel-Fattah Burhan. 

Wakati wa ziara hiyo ya Jumatano (27 Januari), Abiy alikutana pia na viongozi wengine mbalimbali wa kisiasa wa Sudan ambao wengi wao wanashiriki mazungumzo ya kumaliza utawala wa kijeshi uliodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja.