1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ethiopia yaanza kujaza maji kwenye bwawa lenye utata

6 Julai 2021

Ethiopia imeanza awamu ya pili ya kujaza maji katika bwawa kubwa lenye utata katika Mto Nile. Hatua inayozidishamvutano kati ya nchi hizo kuelekea mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala hilo

https://p.dw.com/p/3w7Gi
Staudamm in Äthiopien
Picha: Yirga Mengistu/Adwa Pictures/dpa/picture alliance

Misri kupitia wizara yake ya maji na umwagiliaji, imeshutumu na kuipinga hatua hiyo ya Ethiopia, ikisema ni ukiukaji wa sheria za kimataifa pamoja na kanuni za ujenzi wa miradi katika kingo za mito ya kimataifa.

Bwawa hilo ambalo litakuwa kubwa zaidi barani Afrika la kufua umeme, limekuwa chanzo cha mvutano wa kidiplomasia kati ya Misri, Ethiopia na Sudan kwa takriban muongo mmoja sasa.

Ethiopia inasema mradi huo ni muhimu kwa maendeleo yake. Lakini Misri na Sudan zinahofia bwawa hilo litapunguza maji ambayo raia wao wanategemea katika mto Nile