1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wawili wapoteza maisha mkasa wa kuporomoka jengo Ujerumani

7 Agosti 2024

Waokoaji wameendelea na zoezi la kuwaokoa watu waliokwama baada ya sehemu ya jengo la hoteli moja ya magharibi mwa Ujerumani kuanguka.

https://p.dw.com/p/4jDL4
Juhudi za uokoaji zikiendelea eneo la mkasa
Juhudi za uokoaji zikiendelea eneo la mkasa.Picha: Harald Tittel/dpa/picture alliance

Mamlaka zimesema watu wawili wamekufa na wengine kadhaa wamejeruhiwa. Taarifa ya polisi imesema ghorofa ya pili ya hoteli hiyo iliyoko katika mji wa Kroev, magharibi mwa jiji la Frankfurt ilianguka majira ya 5 za usiku jana Jumanne.

Sababu za ajali hiyo bado hazijajulikana. Msemaji wa polisi katika eneo hilo Joerg Teusch, amewaambia waandishi wa habari hii leo kwamba watu wawili waliokufa ni mwanamke na mwanaume, lakini wengine watano walifanikiwa kutoka, miongoni mwa watu 14 waliokuwemo hotelini hapo.

Mapema leo, vikosi vya uokozi viliwaokoa mwanaume mmoja, mtoto mmoja na wanawake wawili.