1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaEcuador

Watuhumiwa mauaji ya mgombea Urais Ecuador wauwawa gerezani

Angela Mdungu
7 Oktoba 2023

Watuhumiwa 6 mauaji ya aliyekuwa mgombea wa Urais nchini Equador Fernando Villavicencio, wameuwawa wakiwa gerezani jana Ijumaa.

https://p.dw.com/p/4XEtm
Askari wa Ecuador wakiwa katika majukumu ya kulinda usalama
Askari wa Ecuador wakiwa katika majukumu ya kulinda usalamaPicha: GERARDO MENOSCAL/AFP/Getty Images

 Taarifa ya kuuwawa kwa watuhumiwa hao imetolewa na mamlaka ya magereza ya SNAI ikiwa imesalia wiki moja kabla ya kuanza kwa uchaguzi muhimu. 

Mamlaka hiyo imesema tukio hilo limetokea katika jela ya Guayas katika mji wa Guayaquil. Watuhumiwa waliouwawa wametambuliwa kuwa niraia wa Colombia. Rais wa Ecuador Guilermo Lasso amelazimika kusitisha safari yake binafsi jijini New York ili kulishughulikia tukio hilo. 

Soma pia:Ecuador: Mgombea urais auawa kwa kupigwa risasi
 
Mgombea Fernando Villavicencio, aliyekuwa mwandishi wa habari mwenye miaka 59, aliuwawa kwa kupigwa risasi Agosti 9 baada ya kufanya mkutano wa kampeni katika mji mkuu Quito, siku chache kabla ya awamu ya kwanza ya uchaguzi.