1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu wawili wanyongwa kwa kushambulia eneo takatifu Iran

8 Julai 2023

Iran, leo imewanyonga hadharani wanaume wawili, kutokana na kuhusika kwao katika shambulio la Oktoba mwaka jana dhidi ya eneo takatifu kwa madhehebu ya waislamu wa Kishia la Shah Cheragh.

https://p.dw.com/p/4TcNZ
USA l Kundgebung gegen die Hinrichtung von Karami und Hosseini
Picha: Allison Bailey/NurPhoto/picture alliance

Tukio hilo la Oktoba 26 ambalo kundi la itikadi kali linalojulikana kama "Sunni Muslim extrimist Islamic State" lilidai kuhusika nalo lilisababisha vifo vya watu 13 na kujeruhi wengine 30.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na shirika la habari la Iran IRNA, hukumu hiyo ya kifo imetekelezwa leo asubuhi ambapo wawili hao walinyongwa karibu na eneo hilo takatifu kwenye mji wa Shiraz ambao ni makao makuu ya mkoa wa Fars.

Soma zaidi:Amnesty: Idadi ya watu walionyongwa iliongezeka mwaka 2022 

Watu hao waliotambulishwa kwa majina ya  Ramez Rashidi na Naeem Hashem Qatali walihukumiwa adhabu hiyo mnamo mwezi Machi mwaka huu kwa makosa ya rushwa, uasi wa kutumia silaha na kwa kujihusisha na vitendo vinavyotishia usalama wa taifa. Washukiwa wengine watatu katika kesi hiyo walihukumiwa kifungo cha miaka 15 na 25 gerezani.