1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya walaani kunyongwa kwa wanaume watatu Iran

20 Mei 2023

Umoja wa Ulaya umelaani vikali hatua ya Iran ya kuwanyonga watu watatu waliokutwa na hatia ya kuwaua askari wa vikosi vya usalama wakati wa maandamano ya kupinga serikali

https://p.dw.com/p/4RbLP
Symbolbild | Galgen und Schlinge
Picha: Allison Bailey/NurPhoto/picture alliance

Ofisi ya mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell imetoa wito kwa mamlaka za Iran kujizuia katika kutekeleza adhabu ya kifo katika siku za usoni.

Wanaume watatu Majid Kazemi, Saleh Mirhashemi na Saeed Yaghoubi wamenyongwa siku ya Ijumaa baada ya kukutwa na hatia ya mauaji ya maafisa watatu wa usalama. Shirika la Kimataifa la Amnesty International, pamoja na makundi mengine ya kutetetea haki za binadamu yameorodhesha mateso ya waandamanaji waliotiwa kizuizini.

Mauaji hayo ya Ijumaa, yamefanya idadi ya watu walionyongwa kuhusiana na maandamano kufikia watu saba. Mamlaka za Iran zilikandamiza maandamano makubwa yaliyozuka kutokana na mauaji ya msichana wa Kikurdi Mahsa Amini mnamo Septemba 16.