1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu Wanane wauwawa katika shambulio la kanisa Ethiopia

29 Desemba 2023

Watu wanane wameuawa na wengine watano wamejeruhiwa kufuatia shambulio la anga kwenye Kanisa moja katika jimbo la Oromia nchini Ethiopia.

https://p.dw.com/p/4aiVe
Ethiopia | Mkutano wa waandishi wa habari na jeshi la polisi
Jeshi la polisi likiwa katika mkutano na waandishi wa habari ambao hawapo pichani, likitoa taarifa kuwakamati wapiganaji kadhaa wa OLAPicha: Messay Teklu/DW

Hayo yameelezwa na mashuhuda wawili wa tukio hilo pamoja na maafisa wa chama kimoja cha upinzani nchini humo.

Kanisa la Baro Full Gospel huko Horo eneo la Gudru Wellega, karibu kilomita 200 kaskazini magharibi mwa mji mkuu Addis Ababa lilishambuliwa siku ya Jumatatu.

Msemaji wa serikali ya Ethiopia, Legesse Tulu, ametupilia mbali madai hayo ya shambulio la anga na kusema ni "uongo mtupu".

Soma pia:Abiy na kundi la OLA walaumiana juu ya mauaji ya Oromiya

Mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Ethiopia na waasi wa Jeshi la Ukombozi wa Watu wa Oromo (OLA) ambayo yanalenga kumaliza miongo kadhaa ya mzozo, yalimalizika bila makubaliano mwezi Novemba, na kusababisha kutokea mashambulizi ya hapa na pale huko Oromia ambalo ni eneo kubwa zaidi nchini humo.