1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Abiy awatuhumu waasi wa Oromo kufanya mauaji ya kimbari

5 Julai 2022

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amewatuhumu waasi wa jamii ya Oromo kwa kufanya mauaji mapya ya "halaiki" katika eneo moja lenye hali dhaifu ya usalama na ameahidi ataliangamiza kundi hilo.

https://p.dw.com/p/4Dh8C
Äthiopien ehrt seine Polizeikräfte
Picha: Michael Tewelde/XinHua/dpa/picture alliance

Katika ujumbe aliouandika kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, Abiy, amesema raia wanaoishi kwenye eneo la Qellem Wollega katika jimbo la Oromia wameuwawa kwa idadi kubwa.

Waziri mkuu huyo anasema kundi la Ukombozi wa Waoromo OLA ambalo limeorodheshwa na serikali yake kama kundi la kigaidi, linawahangaisha raia wakati wapiganaji wake wanakimbia mashambulizi ya vikosi vya usalama Oromia magharibi.

Taarifa hiyo ya waziri mkuu Ahmed haijaweza kuthibitishwa kwa sababu njia ya kuelekea eneo la Oromia Magharibi zimefungwa na mawasiliano katika eneo hilo alilolitaja Abiy yametatizika.