1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sitini wahofiwa kufariki Ukraine

Hawa Bihoga
9 Mei 2022

Zaidi ya watu 60 wanahofiwa kufariki baada ya bomu la Urusi kuangukia shule iliokuwa ikitumiwa watu kujihifadhi, huku vikosi vya Moscow vikiongeza mashambulizi katika kiwanda cha chuma mjini Mariupol.Ukrein ilisema

https://p.dw.com/p/4B1VU
Ukraine | Mariupol - Zivilisten verlasssen zerstörte Gebäude
Picha: Peter Kovalev/TASS/picture alliance

Vikosi vya Urusi ambavyo vimeonekana kusonga mbele katika mji wa Mariupol viliendeleza mashambulizi makali leo asubuhi katika maeneo muhimu ya mji huo, ikiwa ni sehemu yake ya kupata ushindi katika mapigano hayo ambayo bado jumuia za kimataifa zinaendelea kuisaka suluhu.

Mamlaka za Ukraine zilisema takriban watu 90 walijificha katika ghorofa ya chini, kikosi cha uokoaji nchini humo kilipata miili ya watu wawili na kuokoa wengine 30, lakini ilitilia mashaka kwamba wengine 60 wamefunikwa na kifusi hivyo tumaini la watu hao kusalia hai ni dogo.

Soma pia:Biden atangaza shehena mpya ya silaha kuisaidia Ukraine

Mashambulizi ya Urusi ambayo yanaendelezwa katika maeneo muhimu nchini Ukraine pia yamewauwa wavulana wawili wenye umri wa miaka 11 na 14 katika eneo la mji wa Pryvillia sehemu ya Donbas ambayo nikitovu cha viwanda ambayo majeshi ya Urusi yanalenga kuudhibiti.

Manusura wakabiliana na hali ngumu ya kiutu

Walionusurika katika eneo hilo walisema walikabiliana na hali ngumu katika makazi hayo kutokana na kusikika makombora ya mara kwa mara kwa vikosi vya Urusi, upungufu wa chakula na hata mazingira magumu katika maeneo hayo.

Ukraine, Saporischschja | Evakuierung aus Mariupol
Manusura waliookolewa kutoka MariupolPicha: Francisco Seco/AP/dpa/picture alliance

Volodymyr Babeush aliema tumaini lao lilikuwa ni siku moja wataondoka  katika eneo hilo na kuwa katika eneo salama.

" Tulifanya majaribio kadhaa ya kutoroka lakini hayakufanikiwa" Alisema hukuakionekana kuwa amepata tumaini jipya baada ya kuishi katika mazingira magumu kwa muda mrefu.

" Hatimae tumehamishwa. tunawashukuru" alimalizia kusema huku akiingia kwenye gari kuanza safari kwa ajili ya kupelekwa katika maeneo mengine salama.

Soma pia:Vita vya Ukraine: Urusi yaendeleza mashambulizi katika kiwanda cha chuma cha Azovstal

Mabasi takriban 10 yaliwasili katika eneo hilo yakiwa na raia 174 waliohamishwa kutoka maeneo tofauti ya mji ulioshambuliwa wa Mariupol. Mmoja ya waliookolewa alinukuliwa akisema:

Hata hivyo, mamia ya watu wengine ambao walikuwa na matumaini ya kujiunga na msafara huo wa uokoaji kutoka maeneo mengine ambayo kwa sasa yanashikiliwa na vikosi vya Urusi walilazimika kusalia kwenye maficho yao baada ya Urusi na Ukraine kushindwa kufikia makubaliano juu ya njia za kiutu zinazotumika kuwahamisha raia.

Umoja wa Mataifa walaani shambulio hilo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amesema ameshtushwa kufuatia shambulio hilo la shule lililoripotiwa siku ya Jumamosi katika kijiji cha mashariki cha Bilohorivka na kulitaja kuwa ni ishara nyingine kwamba raia ndio wanaathirika zaidi katika vita hivyo vilivyoanza mwishoni mwa mwezi Februari.

Wa-Ukraine waapa kutetea maeneo yao

Leo Jumatatu wakati Urusi ikiadhimisha Siku ya Ushindi, vikosi vyake vimeendelea kusonga mbele na mfululizo wa mashambulizi wakilenga kudhibiti eneo muhimu la mji wa bandari wa Mariupol, ikilenga kupata mafanikio ya ushindi katika vita hivyo ambayo vimeingia wiki ya 11 sasa.

Soma pia:Mapambano makali yaripotiwa kiwandani Mariupol

Majeshi ya Urusi yalikishambulia kiwanda cha chuma cha Ukraine ambapo wapiganaji wa Ukraine takriban 2,000 wameendelea kuupigania mji wa Mariupol ulioharibiwa vibaya.