1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu laki Moja watanufaika na madawa ya UKIMWI Nigeria.

25 Februari 2005
https://p.dw.com/p/CFb7

ABUJA.

Serikali ya Nigeria inakusudia kugawa dawa kwa watu wanaosibika na maradhi ya ukimwi nchini humo, lakini hatahivyo inahofiwa kwamba watu wengi hawatanufaika na mradi huo .

Waziri wa afya wa nchi hiyo amesema kwamba watu laki moja watapatiwa dawa hizo zilizowekewa ruzuku mnamo mwaka huu.

Kwa sasa ni watu alfu 14bbtu wanaopata dawa hizo kwa bei ya dola saba kwa kila mgonjwa kwa mwezi.

Kwa mujibu wa takwimu, Nigeria ina watu wapatao milioni tatu na nusu wanaougua ugonjwa wa ukimwi.

OTTAWA.

Canada Imesema haitashiriki katika mpango wa Marekani wa kujenga ulinzi dhidi ya makombora na badala yake itaimarisha ulinzi wake kwa mujibu wa mapendekezo yaliyotolewa katikabunge la nchi hiyo.

Hatahivyo waziri mkuu wa canada bwana Paul Martin amehakikisha kwamba nchi yake itaendelea kufungamana na Marekani katika harakati za kupambana na ugaidi duniani.