1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 6 wajeruhiwa katika shambulio jipya la kisu Ujerumani

Angela Mdungu
31 Agosti 2024

Kwa mujibu wa polisi, mtuhumiwa katika tukio hilo lililotokea Ijumaa (30.08.2024) jioni ni mwanamke mwenye miaka 32 raia wa Ujerumani na tayari amekamatwa.

https://p.dw.com/p/4k82I
Polisi wamshikilia mwanamke wa miaka 32 aliyehusika na shambulizi la kisu lililowajeruhi watu sita mjini Siegen
Polisi wamshikilia mwanamke wa miaka 32 aliyehusika na shambulizi la kisu lililowajeruhi watu sita mjini SiegenPicha: Rene Traut/IMAGO

Shambulio hilo lilifanywa wakati basi hilo likiwa limebeba abiria 40 waliokuwa safarini kuelekea katika tamasha la kusherehekea miaka 800 tangu kuanzishwa kwa miji huo.

Taarifa ya polisi imeeleza kuwa bado wanafanya uchunguzi ili kubaini sababu ya uhalifu huo. Hata hivyo imesisitiza kwamba, hakuna ishara yoyote kuwa shambulio hilo lilikuwa la kigaidi.

Tukio hilo limefanyika ikiwa ni wiki moja tangu mtu mmoja alipofanya shambulio la aina hiyo na kuwauwa watu watatu katika mji wa Solingen, magharibi mwa Ujerumani.