1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 5 wauawa kwenye shambulizi Kongo

13 Mei 2023

Watu watano wameuawa katika shambulizi lililotokea magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

https://p.dw.com/p/4RJ6L
Kongo I Soldaten während einer gemeinsamen Militäroperation gegen bewaffnete Kräfte in Beni
Picha: Alain Uaykani/Xinhua News Agency/picture alliance

Msemaji wa jimbo la Kwango, Adelar Nkisi amesema wapiganaji wa Mobondo walikishambulia kijiji cha Batshongo, Ijumaa usiku. 

Nkisi amesema kwamba wanajeshi wawili, askari polisi mmoja na raia wawili wameuawa katika shambulizi hilo, akisema kuwa wanajeshi hao walikatwa vipande vipande.

Symphorien Kwengo, kiongozi wa kiraia wa Kwango, amesema kwamba mapigano kati ya wapiganaji wa Mobondo na vikosi vya usalama yalisababisha vifo vya takribani watu wanne.

Siku ya Alhamisi, mwanajeshi mmoja na wanamgambo wanne waliuawa katika shambulizi linalodaiwa kufanywa na Mobondo katika kijiji cha Nguma kwenye jimbo la Kinshasa.