1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 42 wauwawa na waasi wa ADF nchini Kongo

14 Juni 2024

Wapiganaji wa kundi la kigaidi ADF wamewauwa watu 42 katika kijiji cha Maikengo kwenye utawala wa Bapere wilayani Lubero na idadi hiyo huenda ikaongezeka. Mauaji hayo ni ya kwanza kufanyika katika eneo la Bapere.

https://p.dw.com/p/4h2dC
DR Kongo
Wapiganaji wa kundi la ADF ladaiwa kufanya mauaji ya wengi katika eneo la Bapere, DR KongoPicha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Kiongozi wa Bapere, Makere Sivikunula Mwendovwa, alitangaza idadi hiyo ambayo huenda ikaongezeka kwani, kila wanapofanya mauwaji wanaendelea kuwauwa watu wengine wakielekea katika eneo jengine. 

Mauwaji katika kijiji cha Maikengo wilayani Lubero, yanafuatia yale ya Cantine, magharibi mwa wilaya ya Beni, ambako wapiganaji wa ADF waliwauwa watu wasiopungua mia mbili wiki iliyopita.

Idadi ya vifo yaongezeka hadi 41 kufuatia shambulio mashariki mwa Kongo

Mashambulizi yanayofanywa na ADF katika mikoa ya Kivu ya Kaskazini pamoja na Ituri, yamegharimu maisha ya maelfu ya raia nchini Kongo.

Ili kukabiliana na mauwaji pamoja na vita vya M23 katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini, mkuu wa majeshi ya Congo jenerali Tshiwewe Songisa alikutana jana mjini Goma kwa mazungumzo maalumu na makamanda wa operesheni katika mkoa huu.