1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiBurkina Faso

Watu 19 wauawa Burkina Faso kwenye shambulizi la wanamgambo

13 Februari 2023

Watu 19, wameuwa nchini Burkina Faso na wasamaria wema tisa kujeruhiwa. Ni kufuatia mashambulizi mawili yaliyofanywa na wanamgambo wenye itikadi kali

https://p.dw.com/p/4NQnt
Dorf im Norden von Burkina Faso
Picha: Michele Cattani/AFP/Getty Images

Afisa mmoja wa ngazi ya juu ameliambia shirika la habari la AFP kwamba miongoni mwao ni watu saba ambao ni wanchama wa kikosi cha wasamaria wema VDP waliouawa Alhamisi usiku wakati Kijiji cha Dembo kilichoko kaskazini magharibi mwa nchi kiliposhambuliwa.

Hapo jana, kundi linalodaiwa kuwa la  kigaidi liliwaua watu 12 wakiwemo wanachama wawili wa VDP katika Kijiji cha Yargatenga, kilichoko mashariki, mpaka wan chi hiyo ya Togo na Ghana. Hayo ni kulingana na duru katika eneo hilo.