1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 18 wameuwawa katika mashambulizi Burkina Faso

6 Februari 2023

Watu 18 wameuwawa katika mashambulizi mawili nchini Burkina Faso, huku ghasia zikiendelea kushuhudiwa katika taifa hilo la Sahel.

https://p.dw.com/p/4N8eX
Burkina Faso | Armee Putschisten Traore
Picha: Kilaye Bationo/AP/dpa/picture alliance

Duru za kiusalama zimethibitisha kutokea kwa shambulio lakini hazikutoa idadi ya waliouwawa.

Siku ya Jumamosi, wanajeshi sita waliuawa katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo, baada ya kukanyaga bomu lililotegwa ardhini.

Kutetereka kwa hali ya usalama katika taifa hilo la Afrika Magharibi kunakosababishwa na makundi ya itikadi kali, kumezusha hasira ndani ya jeshi.

Burkina Faso ilishuhudia mapinduzi mara mbili katika 2022, ya mwisho yakiwa ya mwezi Septemba, wakati Kapteni Ibrahim Traore mwenye umri wa miaka 34 alipotwaa madaraka.