1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfilipino

Ufilipino yaapa kulinda mipaka yake kwa njia ya diplomasia

24 Julai 2023

Rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos Jr. amesisitiza azma ya serikali yake kuilinda mipaka yake kupitia diplomasia katika hotuba yake ya leo kuhusu hali ya taifa.

https://p.dw.com/p/4UK5q
Philippinen Präsident Ferdinand Marcos Jr.
Picha: Sean Kilpatrick/empics/picture alliance

Hata hivyo hakuitaja China, ambayo imekuwa ikifanya msururu wa vitendo vya kuongeza mivutano katika Bahari inayogombaniwa ya Kusini mwa China.

Marcos pia ametangaza katika hotuba hiyo aliyoitoa bungeni kuwa atatoa msamaha kwa wanamgambo wanaoendesha uasi na kufanya msako dhidi ya walanguzi na wanaohodhi bidhaa za kilimo, ambao amewalaumu kwa kuongezeka kwa bei za chakula.,

Soma pia:Ufilipino yaamuru kukamatwa tena kwa mshukiwa wa mauaji

Licha ya msururu wa matatizo na hali ya sintofahamu inayosababishwa kwa sehemu na vita vya nchini Ukraine, Marcos amesema hali ya kujitolea na uzalendo aliouona miongoni mwa wafanyakazi wa Ufilipino ndani na nje ya serikali umemfanya kuwa mwenye matumaini.