1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSyria

Watu 112 wauawa katika shambulio nchini Syria

6 Oktoba 2023

Zaidi ya watu 110 wameuawa hapo jana katika shambulio dhidi ya chuo cha kijeshi nchini Syria, na wengine zaidi ya 200 wamejeruhiwa.

https://p.dw.com/p/4XBJp
Syrien I Rauch über Qamishli
Picha: Orhan Qereman/REUTERS

Hayo yanajiri wakati Uturuki imekuwa ikiendeleza pia mashambulizi dhidi ya maeneo ya Wakurdi nchini humo na kusababisha vifo vya takriban watu 11.

Jeshi la Syria limeahidi kujibu vikali shambulio hilo lililotokea wakati wa sherehe za kupandishwa cheo kwa maafisa wa serikali huko Homs, na kusema limetekelezwa na makundi ya kigaidi kwa kutumia ndege zisizo na rubani zilizojazwa mabomu. Hadi sasa hakuna kundi lililodai kuhusika na tukio hilo.

Geir Pedersen, mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya  Syria amesema katika taarifa yake kuwa matukio hayo ya kutisha ni ukumbusho wa haja ya kukomesha mara moja ghasia, kuwepo usitishaji vita nchi nzima na mbinu ya ushirikiano katika kukabiliana na makundi ya kigaidi.