1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watoto 4 wafa, 15 wajeruhiwa kwa kuangukiwa na kanisa

16 Oktoba 2023

Watoto wanne wamekufa na wengine kumi na watano wamejeruhiwa baada ya kuangukiwa na jengo la kanisa lililoporomoka kutokana na mvua kubwa kusini mwa Burundi.

https://p.dw.com/p/4XaYS
78th UN Vollversammlung Afrika Evariste Ndayishimiye Burundi
Rais Evariste Ndayishimiye wa Burundi.Picha: BRENDAN MCDERMID/REUTERS

Watoto wanne wamekufa na wengine kumi na watano wamejeruhiwa baada ya kuangukiwa na jengo la kanisa kusini mwa Burundi ambalo lilibomoka kufuatia mvua kubwa zilizonyesha siku ya Jumapili (Oktoba 15) eneo hilo.

Mkasa huo ulitokea huko Kiyange karibu na mpaka wa Burundi na Tanzania.

Soma zaidi: Mfumo wa ukabila wapingwa Burundi

Mamlaka eneo hilo imefahamisha kuwa Shirika la Msalaba Mwekundu la Burundi kwa ushirikiano na shirika ulinzi wa raia pamoja na wakaazi, wameendelea na zoezi la uokozi.

Taarifa hiyo imethibitishwa pia na vyombo vya habari vya Burundi.

Kulingana na Benki ya Dunia, taifa hilo la Afrika Mashariki lililo katika eneo la Maziwa Makuu ndiyo nchi masikini zaidi duniani.