Hofu yatanda Msumbiji kabla ya maandamano ya upinzani
6 Novemba 2024Kumeshuhudiwa wiki kadhaa za maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi ambayo yamesababisha vifo vya watu 18.
Maduka na mabenki mjini Maputo yalifungwa mapema leo na mitaa haikuwa na watu. Magari ya polisi na jeshi yaliwekwa katika maeneo tofauti ya mji.
Nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika imekuwa na mgogoro wa kisiasa tangu tume ya uchaguzi ilipotangaza kuwa chama cha Frelimo, ambacho kimekuwa serikalini kwa karibu miaka 50, kilishinda uchaguzi wa Oktoba 9.
Soma pia:Makabiliano Msumbiji polisi ikitawanya maandamano ya uchaguzi
Mondlane, ambaye yuko mafichoni, ameandika kwenye mitandao ya kijamii kuwa atashiriki katika maandamano hayo.
Shirika la Human Rights Watch lilisema vikosi vya usalama viliwauwa waandamanaji 18 tangu uchaguzi huo.
Nacho Kituo cha Demokrasia na Haki za Binaadamu - CDD kimesema watu 24 waliuawa katika ukandamizaji wa polisi dhidi ya waandamanaji. Amnesty International leo imeihimiza serikali kusitisha ukiukaji wa haki za binaadamu na kuheshimu haki za kila mmoja kujieleza na kukusanyika kwa amani.