Machafuko yaendelea kushuhudiwa Msumbiji
3 Novemba 2024Matangazo
Machafuko yamelikumba taifa hilo la Kusini mwa Afrika tangu kumalizika kwa uchaguzi mnamo Oktoba 09 ambao ulikipa ushindi chama tawala cha Frelimo kilichokuwa madarakati tangu mwaka 1975 lakini ukilaaniwa na vyama vya upinzani vinavyodai kuwepo na udanganyifu.
Soma pia:Chama kikuu cha upinzani nchini Msumbiji chaomba kura kuhesabiwa upya
Asasi moja ya kiraia imeliambia shirika la habari la AFP kwamba katika mkoa wa Nampula ambao ni kitovu cha machafuko polisi ilitumia nguvu kuwatawanya waandamaji ikiwemo mabomu ya kutoa machozi.
Polisi haijazungumza chochote kuhusu shutuma za kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji.