1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Wasiwasi waongezeka Marekani kabla ya mkutano kuhusu madeni

22 Mei 2023

Wasiwasi umeongezeka huko Washington ambako Rais Joe Biden anatarajiwa kukutana na spika wa baraza la wawakilishi kutoka upande wa chama cha Republican kuhusu majadiliano ya kuongeza viwango vya deni la taifa.

https://p.dw.com/p/4RfxT
US-Präsident Biden Rede zu Schuldenerlass für Studenten
Picha: Evan Vucci/AP/picture alliance

Mkutano huo unakuja chini ya wiki mbili kabla ya muda muhimu wa mwisho uliowekwa kwa Marekani kuepuka kuingia katika janga la kuwa Muflisi.

Soma pia:Biden aakhirisha ziara za nje kwa mzozo wa madeni 

Rais Biden alilazimika jana Jumapili  kuikatisha ziara yake barani Asia na kurejea Marekani kuanzisha tena mazungumzo hayo kabla ya Juni Mosi ambayo ni tarehe ya mwisho iliyowekwa na wizara ya fedha ya Marekani ya kulitaka bunge liidhinishe hatua ya kuipatia serikali uwezo wa kukopa zaidi.