1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden aakhirisha ziara za nje kwa mzozo wa madeni

17 Mei 2023

Rais Joe Biden wa Marekani atashiriki katika mkutano wa kilele wa G7 nchini Japan, lakini ameakhirisha ziara yake katika nchi za Papua New Guinea na Australia kutokana na mzozo wa deni nchini mwake.

https://p.dw.com/p/4RUIZ
USA Washington | Schuldenstreit | Joe Biden
Picha: Evelyn Hockstein/REUTERS

Ikulu ya Marekani imesema Biden anaelekea Japan hii leo Jumatano (17 Mei) na atarejea nchini siku ya Jumapili, baada ya kukamilika kwa mkutano wa G7, ili kushiriki kwenye mikutano na viongozi wa bunge la Marekani kuhakikisha kwamba bunge linachukua hatua muafaka ili kuiepusha nchi hiyo na mzozo wa kushindwa kulipa deni lake la taifa.

Spika Kevin McCarthy kutokea chama cha Republican amewaambia waandishi habari kwamba yeye na Rais Biden bado hawajafikia mapatano juu ya suala la kuiwekea serikali kikomo cha kukopa.

Serikali ya Biden inataka iruhusiwe kuendelea kuchukua mikopo wakati wajumbe wa chama cha Republican wanataka matumizi ya serikali yakatwe.