1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Mahabusu wa jela za Marekani watalindwa kwa mujibu wa mkataba wa Geneva

12 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG8I

Wizara ya ulinzi ya Marekani imetoa taarifa kwamba mahabusu wote kwenye jela zote za Marekani duniani lazima waangaliwe kwa mujibu wa mikataba ya Geneva inayowalinda mateka wa kivita.

Hatua hii imekuja wiki mbili baada ya mahakama kuu ya Marekani kuamua kwamba utawala war ais Bush unaohusika na kuwazuilia wafungwa katika jela ya Guantanamo Bay Cuba ulikiuka sheria za Marekani na za kimataifa juu ya kuwalinda mahabusu.Akiushutumu hatua ya rais Bush juu ya suala hili seneta wa chama cha Demokrats katika bunge la marekani Charles Schumer amesema.

Rais huyo amekuwa kama ni tembo anyecheza katika duka la sahani na ameharibu vita vyote dhidi ya ugaidi.Alikuwa hana haja ya kupata hukumu ya koti kuu ili ashauriane na bunge juu ya suala hili.

Kibri kama hicho na kutumia madaraka vibaya siajawahi kukiona katika maisha yangu yote ya kutumikia umma wa Marekani.

Kwa muda wa miezi kadhaa ikulu ya Marekani imekuwa ikishikilia kwamba mikataba ya Geneva ya kuwalinda mateka wa kivita haiwahusu wapiganaji wa kitaliban,Alqaeda wala makundi mingine ya kigaidi.

Wakati huo huo Marekani pia imesisitiza kwamba imekuwa ikizingatia haki za binadamu kwa watuhumiwa wote.