1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Marekani yatishia kuzuwiya mali za Korea Kaskazini

16 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEaa

Marekani yatishia kuzuwiya mali za Korea Kaskazini iwapo nchi hiyo haitokubali kufikia maridhiano kwenye mazungumzo ya nuklea ya nchi hiyo yanayofanyika hivi sasa nchini China kwa kuzishirikisha nchi sita.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleezza Rice amesema Marekani haitegemei mazungumzo hayo pekee kuifanya Korea Kaskazini kuachana na tamaa yake ya kutengeneza silaha za nuklea.Wajumbe katika mazungumzo hayo mjini Beijing ambayo pia yanazijumuisha Korea Kusini,Russia,Japani na China wamekuwa wakijadili pendekezo ambalo litaipatia Korea Kaskazini msaada ili badala yake nchi hiyo ikongowe mipango yake ya kutengeneza silaha za nuklea.

Lakini Korea Kaskazini inataka ipatiwe mitambo mepesi ya nuklea inayoendeshwa kwa nguvu za maji kuzalisha umeme pendekezo ambalo moja kwa moja limekataliwa na Marekani na Japani.