1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Marekani kuiuzia Pakistan ndege za F-16

26 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFTV

Serikali ya Marekani imekubali kuiuzia Pakistan ndege za kivita aina ya F-16.

Hatua hiyo inaonyesha mabadiliko makubwa kwa sera ya Marekani ambayo ilizuwiya kuuza ndege hizo kwa Pakistan miaka 15 iliopita kwa sababu ya wasi wasi juu ya mipango ya nchi hiyo ya kutengeneza silaha za nuklea.

Msemaji wa serikali ya India mjini New Delhi amesema Waziri Mkuu wa India Manmohan Singh amevunjwa moyo sana na uamuzi huo ambapo India imekuwa ikipinga vikali mauzo ya ndege hizo za F-16 kwa nchi jirani ya Pakistan.

Serikali ya India inasema ndege hizo zinaweza kutumika dhidi yake wakati wa mizozo.