1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Adhabu ya kifo kwa vijana yafutwa

2 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFaE

Hairuhusiwi tena kutoa adhabu ya kifo kwa wahalifu walio na umri mdogo nchini Marekani. Hukumu hii imetolewa na mahakama kuu nchini humo na hivyo kusitisha adhabu hii iliyokuwa inaendelea kutolewa katika mikoa 19 nchini humo. Hukumu hii imetengua pia hukumu za vijana 72 -- walioua na wao kuhukumiwa adhabu ya kunyongwa.

Mahakimu wa mahakama kuu wamesema, kwa kutokana na unyama wake, adhabu ya kunyonga watu inakiuka katiba ya Marekani.

Hukumu hii imepitishwa kwa uwingi mdogo wa kura 5 kwa 4. Watu wanaounga mkono adhabu ya kifo wanaukosoa vikali uamuzi huu.