WARSAW:Maadhimisho ya miaka 25 tangu kuundwa kwa Poland Solidarity
1 Septemba 2005Viongozi wa dunia walihudhuria sherehe ya kuadhimisha miaka 25 tangu kuundwa kwa chama cha wafanyikazi wa Poland Solidarity ambapo Poland ilisifika kwa kutoa mchango wake katika kuporomoka ukuta wa chuma na kuungana upya ujerumani.
viongozi wa nchi na serikali walitia saini hati juu ya ujenzi kituo cha mshikamano wa wafanyikazi wa ulaya kitakachokuwa na sehemu ya kumbukumbu na na makao ya utafiti. Sherehe hiyo imefanyika katika kiwanda cha uhandisi wa meli mjini Grandsk Poland.
Wakati huo huo rais wa ujerumani Horst kohler na mwenzake wa poland Aleksander kwasniewski walikumbuka kuvamiwa Poland mwaka 1939.
Katika siku ya tatu na ya mwisho ya ziara yake ya kiserikali huko Poland aliweka shada la maua katika mnara wa makumbusho kukumbuka kuanza kwa vita vya pili vikuu vya dunia.