1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Wapiganaji wenye itakadi kali za kiislamu wamewaua

23 Mei 2023

Wapiganaji wenye itakadi kali za kiislamu wamewaua hii leo watu 6 wakiwamo polisi wanne na walinzi wawili baada ya kuvamia kwa silaha nzito kisima cha kuchimba mafuta na gesi kaskazini magharibi mwa Pakistan.

https://p.dw.com/p/4RhPo
Pakistan | Grenzkorps von Belutschistan
Picha: Banaras Khan/AFP/Getty Images

Afisa wa polisi wa Pakistan Irfan Khan amesema wanamgambo wapatao 50 walivamia Kampuni ya Mafuta na Gesi ya MOL wilayani Hangu karibu na mpaka wa Afghanistan. Hadi sasa hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na shambulio hilo.

Soma pia: Watu 13 wameuwawa katika mapigano Pakistan

Makundi mbalimbali ya wapiganaji, ikiwa ni pamoja na Taliban ya Pakistan, yamekuwa kwa miaka mingi yakiendesha uhalifu kwenye eneo la milima huko kaskazini magharibi mwa Pakistan na kutekeleza mashambulizi dhidi ya vikosi vya usalama na miundombinu.