1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanawake Ujerumani bado hawana nafasi sawa na wanaume

Sekione Kitojo8 Machi 2007

Siku ya Leo Alhamis , ni siku ya kimataifa ya wanawake, na katika siku hii pia , wizara ya wanawake ya serikali ya Ujerumani inasherehekea miaka 20 tangu kuanzishwa. Katika sherehe hizo anahudhuria pia kansela wa Ujerumani Angela Merkel binafsi, ambaye naye aliwahi kuwa waziri katika wizara hiyo.

https://p.dw.com/p/CHIe
Angela ni mmoja kati ya wanawake wachache nchini Ujerumani walioweza kupanda juu
Angela ni mmoja kati ya wanawake wachache nchini Ujerumani walioweza kupanda juuPicha: AP

Kwa mtazamo wa haraka nchini Ujerumani , kila kitu kinaonekana kuwa katika hali nzuri tu. Hususan kwa kuwa ni nchi ambayo inaongozwa na kiongozi mwanamke. Lakini ukiangalia kwa jicho la uchunguzi sana inaonekana wazi kuwa wanawake hawana nafasi sawa kabisa na wenzao wanaume. Hali hii ni lazima pia kansela Angela Merkel aishughulikie.

Kansela Merkel amesema: "Nimeingia madarakani kutokana na kura za Wajerumani na ninawafikiria wote. Nimepata elimu ya Fizikia katika iliyokuwa zamani Ujerumani ya mashariki DDR, na nilikuwa nafanyakazi pamoja na wanaume. Lakini suala la wanawake katika maisha yangu linachukua nafasi ya pekee, ambalo kwakweli sikulitarajia."

Kwamba mada kuhusu wanawake hata katika nchi iliyoendelea kama Ujerumani haijaweza kuondoka katika majadiliano , mtu anaweza kutoa mahesabu. Katika mapampuni 200 makubwa nchini Ujerumani , ni wanawake 11 tu ambao wanakalia nafasi za uongozi, katika makampuni 30 yaliyoorodheshwa katika soko la hisa la Ujerumani DAX hakuna hata mwanamke mmoja aliyeko katika uongozi.

Katika eneo la kisayansi hali ya mambo haina tofauti. Ni kiasi cha aslimia 14 tu cha Maprofesa katika vyuo vikuu vya Ujerumani ni wanawake. Na hii ni licha ya kuwa wanawake kuazia miaka kadha iliyopita wanafanya vizuri sana katika masomo yao ya mwisho katika shule na vyuo vikuu. Wizara ya wanawake inapaswa pia, sio tu kwamba kansela alione tatizo hili, lakini pia wanawake wote katika baraza la mawaziri wanapaswa kulitambua.

Pamoja na kwamba Ulla Schmidt anafikiri kuwa , mtu anaweza kuachilia hali ya mambo iende kwa njia hiyo tu, lakini waziri huyo wa afya kutoka chama cha SPD anapambana tangu miaka alipokuwa kijana kuhusiana na haki za wanawake. "Sijawahi kuacha kufikiria, hata wakati huu ambapo nakaribia kufikia umri wa miaka 60 wa maisha yangu kulijadili suala hili. Kwasababu hadi sasa hakuna usawa kati ya wanawake na wanaume.", alisema Bi Schmidt.

Kuhusiana na mabadiliko katika hali hii , hivi sasa ni kazi ambayo anapaswa kuifanya Ursula von der Leyen. Mwanasiasa huyu kutoka chama cha CDU ni kiongozi katika wizara ya wanawake ambaye anashughulikia masuala ya familia, wazee na vijana. Anajaribu kupambana ili kuwasaidia wote ili kupata hali bora katika mazingira ya familia na kazi. Hili linasababisha tatizo kubwa kwa wanawake na linakuwa msingi wa kwanini Ujerumani hakuna watoto wengi wanaozaliwa.

Tayari kuna majadiliano katika jamii ya Kijerumani kuhusu , iwapo ni sawa, kwa wazazi kuwaacha watoto wao wadogo kwa mama walezi kila siku ama kama si sahihi.