1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanasayansi wawili wa Afrika watunukiwa Tuzo ya Ujerumani

25 Oktoba 2022

Wanasayansi 2 wa Kiafrika wametunukiwa Tuzo ya Ujerumani kwa Afrika ya mwaka huu wa 2022, nao ni Tulio de Oliveira and Sikhulile Moyo. Tuzo hii ni baada ya wao kugundua aina ya kirusi cha omicron mnamo Novemba 2021.

https://p.dw.com/p/4IeMm
Deutscher Afrika-Preis 2022 für Virologen Tulio de Oliveira und Sikhulile Moyo l Bildkombo
Picha: sun / bhp

Sikhulile Moyo kwa hakika ni mmoja wa watafiti mashuhuri wa ugonjwa wa UKIMWI barani Afrika. Kisha janga la Corona linazuka na Bwana Moyo, ambaye ni mkurugenzi wa maabara katika Taasisi ya UKIMWI ya Havard nchini Botswana, anaanza kufanya utafiti kuhusu aina mpya ya kirusi. Mnamo Novemba mwaka 2021, anagundua kitu ambacho kinabadilisha hata maisha yake: aina ya virusi ambayo haikufahamika hapo awali.

Bwana Moyo alisema alipokuwa akirejea katika mahojiano na DW kuwa idadi ya mabadiliko ya virusi hivyo ilikuwa ya kushangaza" . Alilinganisha matokeo yake na utafiti uliopo na kuchapisha data hizo kwenye mtandao. Onyo aliyoitoa kwa aina hiyo mpya ya virusi vinavyoambukiza kwa haraka ilisambaa kote ulimwenguni na kwa muda mfupi, sambamba na aina hiyo ya virusi vya Corona ambavyo Shirika la Afya Duniani (WHO) viliipa jina la Omicron.

Soma zaidi: Aina mpya ya kirusi cha Omicron yaripotiwa

German Africa Prize in 2022 Covid-19 Omicron Variante
Aina ya kirusi cha Omicron.Picha: DW

Kwa ugunduzi huu muhimu katika pambano hilo dhidi ya UVIKO19, Raia huyo wa Zimbabwe anapokea Tuzo ya Afrika ya Ujerumani ya mwaka 2022 pamoja na Tulio de Oliviera kutoka Afrika Kusini, ambaye wakati fulani alikuwa mwalimu wake. De Oliviera mzaliwa wa Brazil alihamia Afrika Kusini alipokuwa na umri wa miaka 21. Kupitia mama yake raia wa Msumbiji, daima alijihisi kuwa na uhusiano wa karibu na bara la Afrika. Leo hii, ni mmoja wa wataalam wakuu wa virusi nchini humo na mtaalamu wa magonjwa ya milipuko.

Kwa tuzo hii, Wakfu wa Afrika wa Ujerumani umekuwa ukiwatunuku watu wa Afrika tangu mwaka 1993 ambao, kwa mtazamo wa jopo la kutoa tuzo hiyo, wamekuwa wakijitolea kwa kudumisha amani, upatanishi na maendeleo ya kijamii. Washindi wa awali ni pamoja na rais wa zamani wa Botswana Ketumile Masire, mwanaharakati wa haki za wanawake wa Somalia Waris Dirie na raia wa Kenya ambaye ni hodari wa sayansi ya kompyuta Juliana Rotich.

Soma zaidi:WHO: Maambukizi ya Omicron barani Africa yamepungua 

Washindi wa mwaka huu, Moyo na De Oliviera, wametokea kuwa maarufu ulimwenguni kote kutokana na ugunduzi wao. Saa chache baada ya Moyo, wanasayansi katika Kituo cha Kudhibiti Mlipuko na Ubunifu cha Chuo Kikuu cha Stellenbosch katika nchi jirani ya Afrika Kusini pia waligundua aina hiyo hatari ya virusi. Tulio de Oliviera anayeongoza kituo hicho karibu na jiji la Cap Town, na ambapo alikuwa akimfundisha Moyo mzaliwa wa Zimbabwe kabla ya kupata shahada ya udaktari mnamo mwaka 2016.

Sayansi ya hali ya juu

3d Darstellung des Coronavirus
Aina ya virusi vya corona (UVIKO19).Picha: Mis/IMAGO

Wanasayansi hao wawili wanafanya kazi kwa ushirikiano. Walikuwa katika orodha ya jarida la Time kwa watu 100 wenye ushawishi mkubwa zaidi kwa mwaka 2022. Oliviera alisema katika mahojiano na DW kuwa ni vizuri kutambuliwa lakini lengo lao si kupata tuzo. ​​Kwamba kinachowaridhisha mno ni kufanya sayansi kwa kiwango cha juu na kuifanya kuwa sera inayoweza kuokoa maisha ya watu. Oliviera amebaini pia kuwa wanajali sana kuwawezesha wanasayansi wengine wa Kiafrika.

Kwa upande wake Moyo, kupokea tuzo hiyo kwa niaba ya wanasayansi wa Kiafrika ni heshima kubwa. Anasema kwamba aina ya kirusi cha Omicron ilifichuliwa kwa kuilinganisha na aina ya virusi vingine kwenye hifadhidata ya umma. Anasema tuzo hiyo inawakilisha watu wengi walio nyuma yao na kusisitiza kuwa bila ushirikiano, wasingekuwa hapo walipo kwa muda huu mfupi.

Ubinafsi wa nchi zilizoendelea

Oliviera pia amefurahishwa na mafanikio ya watafiti wa Kiafrika. Anasema Janga la UVIKO 19 lilionyesha kuwa Afrika inaweza kuwa kinara wa sayansi. Anasema hilo liliwashangaza walio wengi lakini si wao kwa manaa, waliwekeza mno iwe kwa rasilimali watu na vifaa katika miaka 20 iliyopita.

Mwandishi: Schwikowski, Martina / Kriesch, Adrian (DW Afrika)