1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Aina mpya ya kirusi cha Omicron yaripotiwa

Hawa Bihoga
27 Januari 2022

Aina mpya ya kirusi cha Omicron inaripotiwa kusambaa katika nchi za Denmark, Uingereza, India, Sweden na nyingine nyingi. hata hivyo athari ya mabadiliko ya kirusi hicho haijulikani bado.

https://p.dw.com/p/46Blc
SARS-CoV-2 Variante Omicron und COVID-19 Impfstoffe
Picha: Andre M. Chang/Zuma/picture alliance

Pamoja na Demark kuripotiwa kusambaa kirusi hicho kwa kasi serikali ya nchi hiyo imeazimia kufungua kikamilifu shughuli za kawaida kwa kujifunza kuishi na virusi hivyo. 

Tayari inafahamika kutokana na aina ya kwanza ya Omicron inayojulikana kama BA.1 kwamba kirusi hicho kinasambaa kwa haraka zaidi kuliko aina zote za virusi hivyo zilizotangulia, lakini sasa kumezuka aina mpya ya Omicron, ambayo wataalamu wameitaja kama BA.2, imeambukiza watu wasiopungua 400 katika siku za kwanza za mwezi Januari nchini Uingereza na tayari imegundulika katika mataifa mengine zaidi ya 40 duniani.

Soma pia: Wimbi la nne la Covid-19 limefika kileleni barani Afrika-WHO

Orodha ya virusi vya Corona ya PANGO ambayo hurekebishwa mara kwa mara na wanasayansi kutoka vyuo vikuu vya Oxford, Edinburgh and Cambridge inaiyorodhesha Dernmark kama eneo lililoathirika zaidi, kwa kuwa na asilimia 79 ya visa vyote vilivyogundulika hadi sasa, ikifuatiwa na Uingereza ikiwa na asilimia 6, India asilimia 5, Sweden na singapore zikiwa na asilimia 2 kila moja.

Infografik SARS-CoV-2 neue Namen für Varianten EN

Hata hivyo waziri mkuu wa Dernmark , amesema kwenye mkutano wake na waandishi wa hababri kwamba, taifa hilo lipo tayari kuwa la kwanza umoja wa ulaya kufungua mipaka yake licha ya aina hiyo mpya kuendelea kuwepo na serikali yake imeamua isichukulie virusi vya Corona kama ugonjwa hatari.

Kasi ya kusambaa kwa aina hiyo ya kirusi inaonesha kwamba, inaweza kuwa inaambukiza zaidi kuliko aina ya kwanza ya Omicron. Taasisi ya usalama wa afya Uingereza imekiorodhesha kirusi hicho cha BA.2 kama aina mpya ya kirusi kilicho chini ya uchunguzi, waziri wa afya wa uingereza Sajd Javis amesema  kuibuka kwa aina mpya ya kirusi hicho kunaonesha kuendelea kwa umuhimu wa kuchanja.

Soma pia: WHO: Maambukizi ya Omicron barani Africa yamepungua

Hadi sasa maambukizi ya aina ndogo ya kirusi cha BA.2 hayajabainika kuwa makali zaidi  kuliko ilivyokuwa aina ya kwanza ya BA.1 akizungumza na redio ya umma ya Deutschlandfunk mtaalamu wa magonjwa Christian Drosten amesisitiza kwamba, kuunganisha moja ya aina mbili za Omicron na Delta kunaweza kusababisha kuzuka kwa kirusi ambacho ni hatari zaidi.

Mtafiti mmoja wa nchini Cyprus ameripoti hivi karibuni kwamba aina hiyo mpya huenda ikawa ni mchanganyiko wa virusi vyote viwili, hata hivyo ugunduzi wa aina hiyo inayotajwa kuwa ni DeltaCron haujakubalika pakubwa duniani, wataalamu wameendelea kubainisha kuwa ugunduzi huo huenda ulisababishwa na uchafuzi wa sampuli katika maabara.

Nchini Ujerumani bunge limeendelea na mjadala kuhusu muswada wa sheria ambao utaipa mamlaka serikali kuwalazimisha watu wote kuchanja, muswada ambao umeungwa mkono na wanasiasa wa juu kama vile kansela Olaf Scholz ambaye hapo awali walipinga dhana ya kuwalazimisha watu kuchanja. Miongoni mwa mapendekezo yaliyojadiliwa hapo jana ni kuwachanja watu wote wazima pamoja na kuifanya chanjo kuwa ni lazima kwa watu wenye miaka 50 na kuendelea. Wapinzani wa muswada huo wanahoji kuwa kuwalazimisha watu kuchanja ni ukiukwaji wa katiba ya Ujerumani.

Makala hii ilitafsiriwa kutoka kwa Kijerumani